Wanafunzi wa shule ya msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vyakisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiongea kwenye mkutano katika shule hiyo muda mfupi kabla ya kuzindua vyoo hivyo.
Meneja
Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses
akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14,
vitakavyohudumia wanafunzi 850 katika shule ya Msingi ya Makambi, Songea
Mkoa wa Ruvuma, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 4.7 kulia ni
Meneja wa Oparesheni wa tawi la Songea, Simon Mlelwa.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa.
|
Na Mwandishi Wetu
MENEJA mahusiano na mawasiliano wa Benki Posta Tanzania, Noves
Moses amelitaka suala la elimu bure liendane na mazingira mazuri ya kimiundo
mbinu kwa wanafunzi pamoja na walimu wao ili kuifanya elimu hiyo kuwa bora
zaidi.
Moses amelitaka suala la elimu bure liendane na mazingira mazuri ya kimiundo
mbinu kwa wanafunzi pamoja na walimu wao ili kuifanya elimu hiyo kuwa bora
zaidi.
Rai
hiyo aliitoa jana wakati akizindua vyoo vya kisasa vya Shule ya Msingi
ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma, ambavyo vimejengwa na Benki hiyo kwa thamani ya shilingi Milioni 4.7 ikiwa ni sehemu ya mchango kwa jamii katika kuboresha mazingira ya elimu.
Akizindua matumizi ya vyoo hivyo vyenye matundu 14, Noves alisema kuwa jamii na taasisi mbalimbali zinatakiwa zitambue kuwa suala la elimu bure linatakiwa liendane na uboreshwaji wa mazingira ya
wanafunzi na walimu wawapo shuleni hapo.
wanafunzi na walimu wawapo shuleni hapo.
Alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wadau wa elimu kulichukulia suala la elimu bure kama
kigezo cha kutokuchangia sekta hiyo na baadala yake wanadai ni kazi ya
serikali pekee jambo ambalo siyo sahihi katika uboreshaji elimu.
“Suala la elimu bure lisiwe kigezo cha wadau kushindwa kuichangia sekta hiyo kwani kufanya hivyo
kunapelekea baadhi ya shule kushindwa kuwa na mazingira mazuri ya watoto kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na morali ya kufundisha” alisema Meneja mahusiano .
kunapelekea baadhi ya shule kushindwa kuwa na mazingira mazuri ya watoto kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na morali ya kufundisha” alisema Meneja mahusiano .
Noves alisema kuwa Benki ya Posta Tanzania inafanya kazi kwa kiwango kikubwa na serikali
hivyo imetoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa upande wa afya na elimu huku katika upande wa elimu wamechangia madawati na ujenzi wa vyoo bora vya kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .
hivyo imetoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa upande wa afya na elimu huku katika upande wa elimu wamechangia madawati na ujenzi wa vyoo bora vya kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Kanisius Ngongi awali akitoa taarifa ya shule hiyo kabla ya kukabidhiwa vyoo hivyo alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi 850 na matundu ya vyoo yapo 14 na kuwa vyoo vyote vina maji ya kutosha.
Ngongi aliipongeza benki hiyo alisema kuwa shule hiyo kwa sasa imeshabadilika, mazingira
yamekuwa bora kwa upande wa vyoo vya wanafunzi ambavyo kwa sasa hakuna
shule ndani ya Manispaa hiyo yenye vyoo kama hivyo.
Mwalimu Ngongi alisema kuwa licha ya vyoo vya wanafunzi kuwa bora lakini bado kuna changamoto
ya vyoo vya walimu maana vyoo walivyokuwa wakivitumia vimeshapoteza ubora wake na kuwafanya walimu hao kupata shida mahala pa kujisitili hivyo amewaomba wadau mbalimbali waweze kuchangia kama Benki ya Posta inavyojitolea.

Tags
ELIMU