Kuna story zilivuja kwamba Gareth Southgate amepanga kumtema Wayne Rooney kwenye mchezo wa England dhidi ya Slovenia, kocha huyo wa muda wa kikosi cha ‘Simba watatu’ amethibitisha uvumi huo alipozungumza na waandishi wa habari
.
Southgate ametumia busara kufikia uamuzi wa kumweka benchi Rooney akisema kwamba, Eric Dier anafaa zaidi kucheza dhidi ya Slovenia.
Rooney ameunga mkono uamuzi wa kocha wake na amesema, ilikua haizuiliki siku kama hiyo kufika, kama inavyotokea kwa mchezaji yeyote
Akasisitiza kwamba, hakuna kilichobadilika kwake kwa upande wa unahodha na atakuwa akitekeleza majukumu yake kama nahodha akiwa kwenye benchi
Tags
MICHEZO KIMATAIFA