Sergio Aguero aliwapa City goli la uongozi, baada ya kuunganisha mpira mzuri wa Kevin de Bruyne na kufunga goli lake la 150 tangu ajiunge klabuni hapo.
Dondoo muhimu za kufahamu
- City wametoka sare michezo mitatu ya nyumbani mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2009 wakati Mark Hughes alipokuwa kocha wa klabu hiyo.
- Aguero amezifunga timu 28 kati ya 30 tofauti tofauti alizokutana nazo kwenye Ligi Kuu ya England.
- Tangu acheze mchezo wake wa kwanza Premier League Septemba 2015, De Bruyne ametoa pasi za magoli 19 kwenye michuano yote kwa Man City, sita zaidi ya mchezaji yeyote.
- Middlesbrough wameshinda mchezo mmoja tu wa ugenini wa Premier League kati ya 19 waliyocheza (sare mara 5, wamefungwa mara 19).
Tags
MICHEZO KIMATAIFA