Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi
kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia
kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na
mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano
(115) mpaka miaka hiyo 17.
Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa
Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu
aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na
kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha
mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na
aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank
robber)
Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood
watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'!
Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu
mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na
FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza
kumzuia au kumkamata.
Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio
yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua
kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya
kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu
ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEDI"
Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi
ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na
alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa
katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.
Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu
mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio
na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha
nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama
anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo
(majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha,
ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na
fedha..
Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na
alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo
alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na
programu maalum ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana
walioko chuoni! Baada ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda
mfupi kituo cha Fort Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya
kijeshi (Special Forces and tactical weapons training)
Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters
degree ya System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo
ya awali kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics.
Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo
ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi
(third degree black belt)
Baada ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya
mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa 'muhalifu wa daraja la kwanza'
sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na
kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi
kutokea muhalifu professional kama yeye Carl 'the Friday night bank
robber'..
#1: MAANDALIZI KABLA YA TUKIO
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa
mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani
atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi
aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa
matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga
utekelezaji wa tukio moja tu..
Kwanza kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya
kupata orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia
kati ya bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba
ziko pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya
hizo na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko
karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake..
Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya
tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa
kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa
alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa
Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta,
haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!
Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu
ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la
msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia
barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na
kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na
kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu
nukta kwa nukta!
Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia
kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je
hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa
wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha
n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank
husika.. Hapa alitafiti kuhusu 'shifti' zao za kazini, nanj ni teller,
nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma
personality zao..
Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya
maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda
katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa
ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna
yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata
Carl anaeleza Bw. Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua
na kuliona handani mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu
(kumbuka Carl alikuwa na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za
nchi ya marekani)! Inaelezwa kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki
ya Carl ni jinsi yalivyo chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa
vitofali vidogo vidogo.. Pia handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya
juu wa kiwango cha kijeshi (military precision). Ndani ya handaki
kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za
'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura
(first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu,
majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..
Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika
maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake
kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo
akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize
mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio
lenyewe..
#2: UTEKELEZAJI WA TUKIO
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October
au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter
au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama
mapema!
Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..
Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza
kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba
katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika
kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo
inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha
kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini
pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa
distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..
Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote
zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu
kutafuta trail ya alikoelekea!
Now; siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha
usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia
alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na alikuwa
akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa
(crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na
matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa..
Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone
ya ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na
alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii
ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung'amua mtu
wanayemtafuta alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi???
#3 KUVAMIA
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa
anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya
kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..
Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na
wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda
kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye
droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi
ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa
msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl
alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio
karibu..
Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda
usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari
amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..
Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia
kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha
baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na
handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha
alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida
anaendesha baisikeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baisikeli
kwa muda wa kama dakika ishirini au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu
ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri..
then anawek baisikeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na
kuelekea nyumbani..
Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio
la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua
'hela zake'... Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa
ajili ya tukio linalofuata..
#4: KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno! Kuna watoto walikuwa
wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya
huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya
kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa
vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao
wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi,
vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani
ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana
na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa
inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo
wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu
kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi
wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.
FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia
walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate
kumtrack down Carl mpaka wakampata.
Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"
Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa
Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo
uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini
mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa
nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na
FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna
ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya
ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!
Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu
yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..
Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa
huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na
ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema
sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini na naamini
kabisa Hollywood wanaomba usiku na mchana atoke salama ili wamfanye
celebrity na watupe bonge la muvi.!!
Mwisho..
Tags
MAAJABU
