BANDA MEDIA BLOG

Watu wenye silaha washambulia hotelini Nchini Mali

Watu wenye silaha wameshambulia hoteli ya Radisson Blu katika mji mkuu wa Mali, Bamako, ripoti zinasema.
"Kuna dalili kwamba hili ni jaribio la kuwachukua watu mateka. Polisi wako hapo na wamezingira eneo hilo," duru za kiusalama zimeeleza shirika la habari la Reuters.

Milio ya risasi inasikika kutoka nje ya hoteli hiyo yenye vyumba 190, shirika la habari la AFP linasema.
Mwandishi wa BBC Afrique Abdourahmane Dia anasema hoteli hiyo hutumiwa sana na raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Mali.
Agosti, wapiganaji wa Kiislamu waliua watu 13, wakiwemo wafanyakazi watano wa UN, baada ya kushikilia mateka watu katika mji wa Sevare, katikati mwa Mali.
Ubalozi wa Marekani mjini Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba unafahamu kuhusu shambulio hilo na kuwashauri wafanyakazi wake pahala salama nao raia wawasiliane na familia.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG