MKURUGENZI
Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akielezea hatua
wanazopaswa kufanya wajumbe wa Kamati tendaji ya PECA, baada ya kuja
kwa mradi mpya wa uhifadhi wa uvuvi SWIOfish, kwenye mkutano uliofanyika
ukumbi wa Makonyo Wawi Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
WAJUMBE
wa Kamati tendaji wa PECA wakiwa katika kazi za vikundi, ili kuchagua
siku ya kufanya utambuzi wa maeneo ya bahari yenye samaki wa matumbawe
kwa ajili ya mradi wa SWIOfish, kwenye mkutano uliofanyika, ukumbi wa
makonyo Wawi Chake chake Pemba,(Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA
Mtambuzi wa ardhi Pemba Mohamed Salim, akionyesha hati ya kukabidhi
mashamba yaliotambuliwa kwa ajili ya kwenda kwa msajili, ili kisha aweze
kutoa hati kwa wamiliki wa mashamba ambayo yameshatambuliwa, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MRATIBU
wa mradi wa Usimamizi wa uvuvi kusini, magharibi ya bahari ya Hindi
SWIOfish, Ramla Talib Omar akiwasilisha taarifa na malengo ya mradi huo
kwa wajumbe wa kamati tendaji wa PECA, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi
wa makonyo Wawi Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAJUMBE
wa Kamati tendaji ya PECA, wakimsikiliza Afisa Mdhamini Wizara ya mifugo
na uvuvi Pemba, Mayasa Hamad Ali, wakati akifungua mkutano wa
kuwasilisha mradi wa usimamizi wa uvuvi SWIOfish, uliofanyika ukumbi wa
mikutano Makonyo Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).