Jeremia amekuwa msaada mkubwa kwenye klabu yake ya Prisons akiwa amefunga nusu ya magoli yote (Tanzania Prisons imefunga magoli 21 hadi sasa) na kuifanya timu hiyo ya jeshi la Magereza kushika nafasi ya tano ikiwa na pointi 36 kwenye msimamo wa ligi.
Fatilia mahojiano ya kati ya shaffihdauda.co.tz na Jeremia Juma….
Jeremia Juma: Najisikia vizuri sana, inanipa confidence kama mchezaji wa timu ya taifa.
www.shaffihdauda.co.tz: Ulishawahi kufikiria kucheza kwenye timu ya taifa kabla ya kuitwa au nafasi hii imekuja kama zali?
Jeremia Juma: Nikuwa naifikiria sana kucheza timu ya taifa. Siku zote nilikuwa natamani nafasi hii na nilipofikisha mabao 7 nikiwa napata nguvu huku nikiongeza kujituma zaidi na ndipo nilianza kuona ndoto yangu itatimia.
www.shaffihdauda.co.tz: Kwenye timu ya taifa unakutana na washambuliaji wengine wakali kama Maguri, Ajib, Bocco na Samatta, umejipanga vipi kuhakikisha unapata nafasi kwenye kikosi cha Mkwasa? Hata kama siyo kwenye mechi dhidi ya Chad basi kwenye mechi nyingine zijazo
Jeremia Juma: Kila mchezaji anastaili yake uchezaji, mimi nacheza namba 10 au winga-mshambuliaji na aina yangu ya uchezaji inafanana na Ajib na Samatta. Mimi nipo fit na tayari kukabiliana na ushindani wa namba kwenye timu ya taifa.
www.shaffihdauda.co.tz: Nini siri ya mafanikio yako? Kwasababu ni wachezaji wachache ambao wanaweza kufunga zaidi ya magoli 10 wakiwa nje ya timu za Simba, Yanga na Azam
Jeremia Juma: Kujituma uwanjani na kusimamia malengo yangu. Malengo yangu yalikuwa ni kufanya vizuri. Mara nyingi nikichoka uwanjani nafsi yangu huwa inaniambia Jeremia bado hujafunga, najikuta napata nguvu na kujituma zaidi.
www.shaffihdauda.co.tz: Unamalengo gani kwenye soka kwasababu huu ndiyo wakati wako na tayari umeonesha unaweza
Jeremia Juma: Kwasasahivi nataka kupata nafasi kwenye kikosi cha taifa, hilo likiwezekana basi huko kwingine kutakuwa ni rahisi tu.
www.shaffihdauda.co.tz: Unakutana na changamoto zipi kwenye ligi ya msimu huu?
Jeremia Juma: Sasahivi mabeki wananifahamu, nacheewa rafu sana. Kwa mfano tulicheza na Mbeya City nilipigwa kiwiko kiwiko nikapasuka kievu tukacheza dhidi ya Ndanda nikapigwa taya siku mbili nikashindwa kula chakula kigumu, kwahiyo nakamiwa sana.
kwa hisani ya SHAFFIA DAUDA
Tags
MICHEZO KITAIFA