BANDA MEDIA BLOG

HAJI MANARA AMUOMBEA MSAMAHA JERRY MURO KWA RAIS WA TFF


haii
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ameamua kuwa muungwana kwa kumuombea msamaha kwa Rais wa TFF,Jamal Malinzi msemaji wa Yanga Jerry Muro ambaye amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka nchini Tanzania.

Kwako Rais wa TFF
Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi
kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini,
kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba.
Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake,
screen-shot-2016-12-25-at-12-24-43-pm
Ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,
Ninafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba,
Tunamiss rikaka zake zinazoongeza ushabiki na utani wetu wa jadi. kwangu Mh Rais nina hakika utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru,
ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.
Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka. Wako

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG