Watu wakiwa wamesimama kwenye uwanja wa kimat
Wakili
wa zamani wa haki za kibinaadamu, Nana Akufo-Addo, ameapishwa kuwa rais
mpya wa Ghana, katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi kadha wa
Afrika.
Katika hotuba yake ya kwanza,
Nana Akufo-Addo, alimsifu rais anayeondoka madarakani, John Dramani
Mahama, kwa namna alivokiri kushindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Viongozi kadha wa Afrika
walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za
kutawazwa rais mpya, Nana Akufo Addo.
Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra.
Bwana Akufo Addo, aliyewahi kuwa
wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda Rais John Dramani Mahama,
katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa
viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha
kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani.
Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
Tags
SIASA