BANDA MEDIA BLOG

MALINZI AITAKIA KILA LA KHERI YOUNG AFRICANS KESHO DHIDI YA WACOMORO LIGI YA MABINGWA AFRIKA


Malinzi-TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linachukua nafasi hii kuitakia kila la kheri timu ya Young Africans katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo hatua ya awali imeanza wikiendi hii.

Wakati Young Africans inacheza, kesho Februari 12, mwaka huu huku Azam itasubiri mshindi kati ya Mbabane Swallons ya Swaziland na Opara United ya Botswana katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF).
Timu ya Young Africans ambayo ni mabingwa wa Tanzania inayoiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho Jumapili Februari 12, 2017 inacheza naNgaye De Mbe ya nchini Comoro.
“Tunaitakia Wawakilishi wa nchi Young Africans ya Tanzania kila la kheri,” amesema Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG