BANDA MEDIA BLOG

PEPS YAWATAKA WANAFUNZI WA JAMHURI KUACHA KUTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII ILI WAJIEPUSHE KUFANYA VIBAYA KATIKA MITIHANI YAO





Meneja Biashara wa kampuni ya vinywaji ya SBC Tanzania LTD [PEPS] Tawi la Dodoma, Abdala Chuma  akimpa mmoja wa wanafunzi wa  shule ya Jamhuri mjini humo, cheti cha kuhitimu kidato cha sita wakati wa mahafari ya shule hiyo.


Mkuu wa Shule ya Jamhuri ya mjini Dodoma  Mariam Hamis Lubuva akizungumza jambo kwenye mahafari ya kidato cha sita cha shule hiyo

Meneja Biashara wa kampuni ya vinywaji ya SBC Tanzania LTD [PEPS] tawi la Dodoma Abdala Chuma  akifafanua jambo wakati wakati wa mahafali ya kidato cha sita shuleni hapo, kulia ni Mkuu wa shule hiyo Mariam Lubuva na kushoto ni Mwalimu wa Taaluma Isaack Muganda [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]   
Mmmoja wa vijana ambaye hakufahamika jina akifanya ibada wakati mahafali hayo yakiendelea

Wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Jamhuri Sekondari wakisubili kutunikiwa vyeti vya kumaliza katika mahafali  yaliyofanyika shuleni hapo
Wanafunzi wa Shule hiyo wakitoa burudani ya igizo wakati wa mahafali hayo

Burudani na vichekisho  zikiendelea
Wapiga picha wakifuatilia na kuchukua matukio mbalimbali
 
Baadhi ya wahitimu wavulana wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea vyeti vya kuhitimu kidato cha sita
Wasichana wa kidato cha sita katika shule ya Jamhuri wakifurahia jambo mara baada ya kupokea vyeti vya kuhitimu masomo yao

Pongezi ya Kike kwa Mzazi

Pongezi ya kuhimu kidato cha sita huku wengine wakisheherekea na  kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa
Na John Banda, Dodoma
MENEJA Biashara wa kampuni ya vinywaji ya SBC Tanzania LTD [PEPS]  tawi la Dodoma Abdala Chuma amewaonya wanafunzi wa kidato cha sita kutotumia vibaya mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha maandalizi ya mitihani ili kuepuka kufanya vibaya wakati wa  mitihani yao
Meneja huyo ameitoa kauli hiyo wakati alipokuwa  akizungumza kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Jamhuri sekondari ya mjini Dodoma ambapo amewata kuitumia kwa kujiendeleza kitaaluma badala ya kujikita kwenye mambo yasiyo na maadili
“Bado mwezi mmoja tu wa kujiandaa na mitihani hiyo hivyo hakikisheni mnajiandaa kwa kusoma na wale mnaotumia mitandao ya kijamii muitumie vizuri ili iwasaidie kufanya vizuri badala ya kubaki mkitumia kuangalia picha za ngono, wasanii na mambo yasiyo na msingi”, alisema
Aidha Chuma amemshauri Mkuu wa shule hiyo kuziandika changamoto zinaazowakabili kisha akabidhiwe mkuu wa kitengo cha uhusiano cha SBC Tanzania makao makuu ili zifanyiwe kazi kwa kuwa kampuni hiyo kwa sasa inarejesha faida wanazo pata kwa jamii kupitia miradi ya shule
Nae mkuu wa shule hiyo Mariam Hamis Lubuva amesema changamoto walizo nazo ni pamoja na kukosekana kwa uzio, jengo la maktaba, vitabu vya ziada na kiada, vifaa vya maabara kwa ajili ya mchepuo wa sayansi ambapo kwa upande wa wanafunzi swala la utandawazi linasababisha wanafunzi kushuka kitaaluma pamoja na kupolomoka  kimaadili
         

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG