Said Hamisi Ndemla amefunga tena
kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Dodoma
FC dhidi ya Simba uliomalizika kwa Simba kushinda kwa bao 1-0
Ni mara ya pili Ndemla amefunga
goli la aina hiyo, mara ya kwanza aliifunga Polisi Dodoma kabla
haijabadilishwa jina kuwa Dodoma FC. September 3, 2016, Ndemla
alitandika mkwaju wa mbali na kumtungua golikipa wa Polisi Dodoma na
kuiandika Simba bao la pili baada ya Abdi Banda kuwa amefunga goli la
kuongoza.
Kwa maana hiyo, Ndemla ameweka
rekodi ya kuwa mchezaji wa Simba aliyefunga mfululizo kwenye uwanja wa
Dodoma dhidi ya timu moja katika majina tofauti.
Bao la Simba limefungwa dakika ya
69 kipindi cha pili, kocha wa Simba Joseph Omog aliwatumia wachezaji
wengi ambao hawapati nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.
Tags
SIMBA SC