CHADEMA yawataka viongozi wa dini kuendelea kuikosoa serikali ya Tanzania
Wito huo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umetolewa na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Freeman Mbowe alipoongea na waandishi wa habari jijini Dare Salaam na kuwawataka viongozi wa dini kuendelea kuikosoa serikali na wasitishwe na mtu yoyote kwani bila wao kusema jamii ya Watanzania itaangamia.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ametoa kauli hiyo wakati alipozungumzia mambo mbalimbali yanayotokea nchini Tanzania na hali ngumu ya maisha ya Watanzania ilivyokuwa mwaka 2017 uliomalizika jana ambapo aliwanyooshea kidole cha lawama watendaji wa serikali ya Rais John Magufuli.
Aidha Freeman Mbowe amesema: Viongozi wa dini msiingize roho ya uoga, mtaiponya nchi, mkikaa kimya nchi itakufa, nchi inateketea, nchi inaangamia viongozi wa dini msikae kimya watu wanauawa.
Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku chache baada ya serikali kutishia kuwashughulia viongozi wa dini wanaojihusha na masuala ya siasa na kuikosoa serikali ambapo wametakiwa kutojihusha na masuala ya siasa.
Tags
CHADEMA