Poulsen alizaliwa mwaka 1994 huko Copenhagen Denmark, babake alikuwa anafanya kazi kwenye meli ya makontena iliyokuwa inatoka nchi za Afrika kwenda Denmark na katika moja ya safari hizo ndipo alikutana na mama wa mchezaji huyo anayeitwa Lane raia wa Denmark.
Baba mzazi wa mchezaji huyo alifariki kutokana na kansa mchezaji huyo alipokuwa na umri wa miaka sita lakini Poulsen amekuwa akija Tanzania mara kadhaa kumtembelea bibi yake jijini Tanga.
Poulsen anacheza soka la kulipwa katika klabu RB Leipzig inayocheza ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga. Anacheza nafasi ya ushambuliaji, anavaa jezi namba 9 na amewachezea Leipzig jumla ya mechi 156 na kuwafungia mabao 37.
-
Stephan Lichtsteiner mali halali ya Arsenal
-
Tanzania mwenyeji kombe la Kagame, Simba na Young Africans zapangwa kundi moja
Klabu nyingi za Ulaya kama Wolfsburg na Borussia Monchengladbach zimeonesha nia ya kumnunua na mchezaji huyo anatumai kwamba kucheza katika Kombe la Dunia kutamfanya kufahamika zaidi Ulaya.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA