NA JOHN ISRAEL, NANENANE DODOMA
NAIBU waziri wa Kilimo, David Silinde amesema kuwa serikali imejipanga hadi ifikapo mwaka 2030 Itakuwa itimiza lengo lake la kuwa na Matrekta elfu10 ili kumfikia kila mkulima ili aweze kulima kwa tija huku akiwataka wananchi kujitokeza katika maonyesho ya nane nane kujionea teknolojia za kisasa ambazo zitawasaidia.
akiongea mara baada ya kukagua mabanda ya Maonyesho ya zana mbalimbali za Kilimo na kukabidhi Trekta 9 kwa wakulima wa wilaya za Chemba na Kongwa Mkoani Dodoma katika viwanja vya Nane nane Nzuguni, Silinde amesema serikali imejipanga kuwasaidia wakulima wa Tanzania ili Kufikia Kilimo Chenye Tija.
"niwapongeze Wenzetu wa Kampuni ya Pass Leasing kwa kutoa trekta na zana mbalimbali za kulimia kwa wakulima wa Tanzania, leo mmepokea nyie wa kutokea Chemba na Kongwa lakini Mpango wa serikali ifikapo 2030 serikali itakuwa imetimiza kugawa trekta elfu 10 kwa wakulima wetu", amesema
kwa upande wake Mjumbe wa Bodi wa Kampuni ya PASS Leasing, Rosebud Kurwijila amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya utendaji imefanikiwa kuwafikia wakulima zaidi ya 1000 katika maeneo mbalimbali nchini na kuwawezesha zana zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 50 nchini kote.
Mjumbe huyo wa Bodi ya wakurugenzi aliyemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya PASS leasing, amesema Kati ya vijana 20% waliowezeshwa, wanawake ni takribani 10% ambapo Kampuni hiyo imefanikiwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo trekta, powertiller (trekta za mikono), mashine za kuvunia, mashine za kuchakata mazao, magari ya usafirishaji wa mazao ya kilimo na vifaa mbalimbali vinavyotumika kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo,uvuvi na ufugaji.
Aidha amesema kampuni hiyo leo agosti 3,2024 imekabidhi vifaa vya kulimia, ambavyo ni trekta 9 aina ya SWARAJ 744 na SWARAJ 855 zenye themani ya TZS 401.76 millioni kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma toka wilaya ya Kongwa na Chemba waliowezeshwa kupitia huduma za PASS Leasing.
"Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 2000; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 30 na kuwa ameongeza wanufaika takribani 300 kwa kipindi cha msimu mmoja Aidha, katika kanda ya kati, mkoa wa Dodoma na Singida
tumeshawezesha zana zenye jumla ya thamani ya takribani bilioni 13 kwa wajasiliamali zaidi ya 350 kati yao vijana ni 25%" Ameongeza
pia amesema kuwa PASS leasing ikishirikiana na AGRICOM AFRICAPASS Leasing imekuwa na makubaliano ya kibiashara na kampuni ya AGRICOM AFRICA ambao ni wauzaji na wasambazaji wa zana mbali mbali za kilimo ikiwemo trekta, pawatila, machine za kuvunia na zana nyingine.
"Makubaliano haya yanalenga kuhakikisha wakulima wajasiriamali wanapata bidhaa bora, na huduma baada ya mauzo ikiwemo mafunzo na huduma za utengenezaji wa zana.Hadi kufikia sasa kwa kushirikiana na kampuni hii tumeweza kwa pamoja kutoa zana mbalimbali zaidi ya 350, ambazo zipo kwenye ubora wa juu na wakulima wanafurahia huduma zao na Kampuni hii inahudumia wateja nchi nzima kupitia matawi yake yaliyopo Dar es salaam (makao makuu), Melela, Mbeya, Igurusi, Kahama, Mwanza, Sumbawanga na Babati",
Wanufaika wa huduma za PASS Leasing Company Limited, ni mtu binafsi, kampuni na kikundi ambao wamejikita katika shughuli za kibiashara za kilimo, uvuvi, ufugaji wa mifugo na nyuki pamoja na usafirishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo", amesema


