BANDA MEDIA BLOG

watu wawili wapoteza maisha ,16 wajeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa guruneti mjini Kigali, Rwanda


 Na:


Msemaji wa Polisi nchini humo,Theos Badege amesema kuwa baada ya mlipuko huo watu kumi na wanane walijeruhiwa na baadae wawili kupoteza maisha kutokana na majeraha waliyokuwa nayo.
 

Mlipuko huo unaelezwa kutokea jana usiku katika wilaya ya Gasabo,na kuongeza kuwa hakuna washukiwa waliokamatwa wakihusishwa na tukio hilo.
 Vikosi vya usalama vya Rwanda vimekuwa vikilishutumu kundi la waasi la FDLR lenye makazi yake huko Congo DRC hali kadhalika likihusisha maafisa wa zamani wa usalama waishio uhamishoni.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG