Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa baadhi ya viongozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, Prisca Lwangili ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Aidha, Abdallah Hassan Mitawi amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.
Balozi Baraka Luvanda amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, huku Dkt. Franklin Rwezimula akihamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Dkt. Maduhu Kazi naye amehamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Mazingira.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Tags
IKULU