BANDA MEDIA BLOG

ARSENAL MWENDO MDUNDO EPL, YAIKALISHA MAN CITY





Mangala


Magoli mawili yaliyofungwa na Theo Walcott pamoja na Olivier Giroud
yameiwezesha Arsenal kuibuka na pointi tatu kwenye uwanja wao wa
nyumbani dhidi ya Manchester United kwenye mchezo uliochezwa usiku wa
Jumatatu kuamkia Jumanne mchezo uliomalizika kwa Arsenal kuibuka na
ushindi wa bao 2-1.


Kama kawaida yake ‘King of Assists’ Mesut Ozil alitengeneza mabao
yote mawili kabla ya kukwamishwa na wafungaji. Arsenal ilipiga kamba
zake zote kipindi cha kwanza. Goli la kwanza likifungwa dakika ya 33 na
Walcott wakati Giroud yeye alipiga la pili dakika ya 45.


walcott_ozil


Yaya Toure alifanikiwa kuipatia timu yake bao la kufutia machozi
dakika ya 82 kipindi cha pili kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na
beki wa kulia wa timu hiyo Sagna.


Matokeo hayo yanawafanya The Gunners kufikisha pointi 36 ponti mbili
nyuma ya vinara wa ligi hiyo Leicester City ambao wanaongoza ligi wakiwa
na pointi 38 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 17 hadi sasa.
Manchester City bado wataendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na
pointi zao 32 nyuma ya Arsenal.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG