BANDA MEDIA BLOG

SPIKE LEE NA JADA PINKETT SMITH KUSUSIA SHEREHE ZA TUZO ZA OSCARS

Nyota maarufu wawili wa masuala ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wametangaza kususia kuhudhuria tuzo za Oscars kutokana na uteuzi wake kutowakilisha jamii zote.

Muongozaji filamu wa Spike Lee na muigizaji Jada Pinkett Smith wametuma ujumbe kila mmoja wakisema hawatahudhuria utoaji wa tuzo hizo zilizopangwa kufanyika Februari 28.

Tuzo za Oscar zimekumbana na kukosolewa baada ya kuteuliwa watu weupe pekee kuwania tuzo muhimu wakati zikitangazwa Alhamis, hali inayojionyesha kujirudia kwa mara ya pili tangu tuzo zilizopita.

Spike Lee ameandika kwamba hawezi kuunga mkono tena Oscars kwani wanachofanya ni kuwakosea heshima watu weusi na kuhoji kuwa inawezekanaji uteuzi wa wawania tuzo muhimu  20 za uigizaji wote ni watu weupe kwa mwaka wa pili mfululizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG