BANDA MEDIA BLOG

RAIS WA COLOMBIA ATIA SAINI SHERIA KALI YA KUWAADHIBU WANAOSHAMBULIA KWA TINDIKALI

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametia saini sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa wahusika wa matukio ya mashambulizi ya kutumia tindikali.

Sasa mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa la kushambulia mtu kwa kutumia tindikali atahukumiwa kifungo cha jela cha kati ya miaka 12 hadi 50.

Mashambulizi ya kutumia tindikali yamekuwa yakitia hofu kubwa nchini Colombia kwa zaidi ya muongo mmoja.

Watu wapatao 100 wengi wao wakiwa ni wanawake wanakadiriwa kukumbana na mashambulizi ya kutumia tindikali kila mwaka.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG