Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la
mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Gwanseri
wilayani Muleba kuuawa na baba yake wa kambo kisha kumfukia ndani ya
nyumba akiwa amemuweka kwenye mfuko wa plasitiki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amesema tukio la
mwanafunzi huyo kuuawa lilitokea jana katika kijiji cha Karutanga
wilayani Buleba na kumtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Remijius Poncian(16).
Kamanda Olomi amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni baba wa kambo,
Hassan Misigaro (52) anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na
kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Tags
AAH
