Na Peter Mkwavila,Dodoma.
WANYAMA wanaofungwa
majumbani wakiwemo Ng’ombe,Kondoo na Mbuzi wamekuwa kivutio kikubwa katika
maombi maalumu ya kuomba mvua yaliyofanywa na waumini wa dini ya kiislamu kata
ya Chang’ombe ambayo yaliandaliwa na Baraza kuu la bakwata kata hiyo mjini humo.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na mjumbe wa baraza kuu la bakwata kata hiyo Ibrahim Maffita,alisema
kuwa kitendo cha kuwashirikisha wanyama hao ni kama ishara ya kuwakilisha wezao
ambao wanaoishi porini ukizingatia kuwa na wao wanahitaji kupata baraka ya mvua.
Akizungumza na BANDA BLOG mjumbe huyo wa Bakwata kata alisema kuwa kitendo cha kuwaleta wanyama
ni ishara ya kuwawakiisha mbele za Mwenyezi Mungu ili kuwafanikisha kupata mahitaji
wanayoyahitaji kama wanyama wa porini ambayo kwa kupitia mvua hiyo wanaweza
kupata majani na maji.
Kwa upande wake
Alhaji Omary Salumu akitoa hutuba yake kwa waumini hao kwenye ibada hiyo ya maombi,aliwataka
kutumia fursa ya mvua zilizoaanza kunyesha kulima mazao yatakayokomaa haraka
ambayo yatakostahimili kulingana na mvua zinazonyesha kwa mikoa ya kanda ya
kati.
“Ndugu zangu waumini
wa dini ninawaomba tutumie muda huu ambao mvua zimeanza kunyesha kwa kulima na
kupanda mbegu itaayokomaa mapema,badala ya kuyaacha maji hayo yakipita bure ni
vizuri basi yakatumika kwa kulima mazao ambayo yatakayokomaa mapema kwa ajili
ya kupata chakula cha kutosha”alisema.
Naye Alhaji Husseni
Jumbe ambaye ni Shekhe wa kata ya Chang’ombe aliwataka waumini kuendelea na
moyo ya kupenda kufanya ibada mbele za mungu mara kwa mara,badala ya kusubiri
mpaka majanga yatokee na ndipo waweze tukusanyika na kumlilia mwenyezi Mungu.
Alisema kuwa siyo tu
wakati wa majanga ndipo waumini wakutanike na kuungana kwa pamoja juu ya
kumlilia mungu,bali hata pale ambapo hakuna matatizo yoyote wanaweza kukutana
kwa umoja na kuweza kumwomba na yeye akatubariki.
Hata hivyo Shekhe huyo
aliwahimiza waumini kuwa na umoja na kutekeleza haki bila kujali imani ya
mtu,kwa kuwa wakifanya hivyo Mungu atatuletea neema katika nchi yetu pamoja na ardhi
ambayo tumepewa kwa ajili ya matumizi yanayostahili na kupendezwa na mungu
mwenyewe.
Mwisho
Tags
HABARI ZA DINI
