Baada ya kusimama kwa
muda wa takribani wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa
ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam
Sports Federation Cup, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea
tena kesho Jumamosi kwa michezo miwili.
Michezo ya kesho
Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu itakuwa kati ya Mabingwa watetezi wa
VPL, Young Africans na Azam – mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote za Jumamosi,
zitafanyika saa 10.00 jioni.
Ligi hiyo itaendelea
tena kwa siku ya jumapili ambapo wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa
ugenini mkoani Kagera kumenyeana na Kagera Sugar katika uwanja wa
Kaitaba.
Mechi nyingine Mwadui
itakuwa nyumbani ikiwakaribisha maafande wa JKT RUVU ya mkoani Pwani
iliyo chini ya mkurugenzi wa ufundi Abdalah Kibaden kwa wakati huu baada
ya kocha Bakari Shime kujiunga na timu ya vijana ya Serengeti Boys.
Tags
YANGA Vs AZAM