Wakuu, naomba Leo tuweke ushabiki pembeni tudadavue uvamizi wa RC pale
Clouds TV. Naomba tuangalie mazingira yote kwa uwazi kabisa tuje na
conclusive evidence juu ya tukio hilo la kulaaniwa.
1. CCTV FOOTAGE
Anaonekana mkuu wa mkoa akiingia kwenye mlango wa kwanza akifuatiwa na
mtu mmoja aliyevaa kiraia hana silaha kisha askari askari mwenye silaha
aliyefunga mlango huo. Jumla ya walioingia ni watatu. Halafu anaonekani
mkuu wa mkoa akifungua mlango wa pili (wa kuingilia studio?). Anapoanza
kuingia ndani footage inakoma
2. USHAHIDI WA MAZINGIRA
Masaa kadhaa baadaye taarifa zinazagaa kwamba clouds wamevamiwa na mkuu
wa mkoa akiwa na askari wanane wenye silaha na kuwapiga vibaya sana
licha ya kuwatisha watangazaji. Na hapa ndipo shida inapoanzia
...ile footage haithibitishi tykio polite la uvamizi.
*Ukiitazama haioneshi ubabe wowote kwenye kuingia ndani studio. RC aliingia kwa kufungua mlango taratibu
*Nje walikuwapo walinzi ambao hawakushuhudia nia yoyote ya uvamizi mpaka
pale walipopigiwa simu na Ruge (aliyekuwa nyumbani kwake). Wao
walimwona RC akiingia kawaida tu hapo studio.
*Mazingira ya studio ya tv huwa na camera nyingi tu. Ni ajabu sana
kusiwe na kipande japo kifupi cha kile kilichotokea ndani ya studio.
Hats hiyo footage, ni kwa nini inakoma pale tu RC anapoanza kuingia
ndani? Je, ni kweli kuwa clouds wameweka camera hapo mlangoni tu? Au
labda mkuu wa mkoa aliamuru kamera zizimwe kabla ya kuingia ndani?
*Kama kamera zilikuwa mbovu walau tungepata hata audio ya kile
kilichitokea ndani basi. Sio masimulizi tu. Hapo ni studio na vifaa
vyote vipo. Kwa nini tusadiki masimulizi?
3. RIPOTI YA KAMATI
Kamati ilitoa ripoti kwamba RC alivamia akiwa na askari watano? na si
nane. Pia wafanyakazi hawakupigwa kama ilivyoarifiwa hapo awali. Ni kwa
nini ilitolewa taarifa kinzani hapo awali?
4. URAFIKI WA RC NA CLOUDS
Ruge anakiri kuwa hawa ni marafiki wa siku nyingi. Tena anatoa kauli
tata kuwa RC anatabia ya kwenda hapo studio kupiga stori. Swami hapa,
je, kila anapokwenda hutumia utaratibu gani kuingia studio? Je, huwa
anaacha wapi walinzi wake? Kuna rekodi yoyote ya clip za cctv za huko
nyuma ili tuone ilivyokuwa?
5. Kilichopo mpaka sasa ni ushahidi wa masimulizi ya wanaodaiwa
kuvamiwa. Ushahidi wa clip ulikuwa na lengo la kuandaa akili ili
wasikilizaji wafanye mwendelezo wa uvamizi akilini mwao. Mtu wa kwanza
kabisa kuripoti uvamizi huu alipaswa kuwa mlinzi.
Ni mtazamo wangu tu, baada ya tafakuri ya kina. Twende na constructive
criticism kama nilivyofanya mimi, ile timu matusi mkae kando kuruhusu
mjadala. Nawasilisha.
Maswali yatokanayo na mjadala unaoendelea :
**kwa nini Gwajima aliripoti kuvamiwa na kupigwa watangazaji? Nani
aliyewasiliana naye kumpa habari ili alipue? Was it a coordinated move?
**kwa nini clouds hawataki kuripoti tukio hili polisi? Kwa nini
walisubiri liwe magnified na mitandao kwanza? Je, yawezekana walikuwa
wanapima upepo? Je kuna yawezekana kuna ofisi ambayo walitarajia
itaingilia kati ili kulishughulikia suala hili tofauti na vyombo
husika?
**Kwa nini ililazimu waziri kukemea vikali hata kabla ya kujiridhisha
usahihi wake? Kwa nini jinai hii haikuhusisha vyombo rasmi vya
uchunguzi? Kwa nini haikufanyika coordination na mamlak teuzi ya RC?
Kulikuwa na haraka gani ya kukimbilia kwenye press utadhani studio
iliteketezwa? What is behind all this!?
Tags
Paul Makonda
