NA JOHN BANDA, DODOMA
WANAWAKE kata ya Chamwino jijini Dodoma wametakiwa
kuchapa Kazi zitakazowaletea maendeleo ya kiuchumi badala ya kukaa kwenye
mikeka na kupiga soga za Umbea zisizo na faida
Pia wametakiwa kutokuwa na Kiburi
kitakachowasababishia Majivuno kiasi cha kuwavunjia Heshima Waume zao
pindi mambo Yao la yatakapowanyookea.
Hayo Yamebainishwa na Diwani wa Viti Maalumu Jiji la
Dodoma, Mary Nitwa wakati alipokuwa akiwaasa Wajasiriamali zaidi ya 100,
wa Kata ya Chamwino waliofudhu mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za
Ujasiriamali yaliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana kwa
kipindi cha wiki moja.
Diwani huyo Amewaambia Wajasiriamali hao ambao wengi
wao ni wanawake, kwenda kuutumia vizuri Ujuzi walioupata kwenye mafunzo
hayo kwa kuanzisha Biashara zitakazowaongezea kipato, badara ya kupoteza
Muda kwa kukaa kwenye vibaraza na mikeka huku wakipiga umbea na majungu yasiyo
nafaida.
" Acheni mambo ya Umbea na kusemana hovyo,
kaundeni vikundi fanyeni ubunifu wa biashara makachape Kazi Mpate baraka kwa
Mungu, lakini angalizo langu mtakapofanikiwa nyie mlioopo kwenye Ndoa
Msiwadharau waume zenu kutikana na kiburi cha mafanikio, Mungu hapendi ataondoa
baraka zake bure", amesema na kuongeza.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Chamwino Jumanne
Ngede, ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye kufunga Mafunzo hayo
amemuagiza Mtendaji wa kata na Afisa maendeleo ya jamii, kuhakikisha
wajasiriamali hao Wanapata soko la kuuza Keki hasa kwenye sherehe zote
zinazofanyika kwenye kata hiyo.
"Jiungeni vikundi watu wa Benki wapo hapa
mkapewe mikopo yenye Riba ndogo, anzisheni biashara na wale wanaotengeneza Keki
hata Kama wote hapa, nawaagiza kata muwatengenezee mazingira hawa kwenye
sherehe zote zikiwemo harusi hawa ndiyo watengeneze na kuuza keki",
amesema
Ameongeza kuwa kufanikiwa siyo kigezo cha kiburi na
dharau kwawenzi katika ndoa “mimi hapa nilipo nina mashine a kusaga katika
meneo mbalimbali, nina magari ya kutembelea na kufanyia kazi, hata fedha si
haba ninazo lakini mbana sigombani na mama yenu pale nyumbani, na nyie
mkizipata msije makaota mapembe kwa wenzi wenu zitakuja kukimbia bure
ninawaonya”, amesema
Sehemu ya Wahitimu wa mafunzo hayo wakakabidhiwavyeti vya ushiriki na Diwani wa Kata ya Chamwino Jumanne Ngede