NA JOHN BANDA, DODOMA
TUME ya Utumishi wa Mahakama imewaelekeza Wananchi
wenye malalamiko ya Ukiukwaji wa maadili yaliyosababisha kutotendewa haki
katika Maamuzi ya Kimahakama na baadhi ya Maafisa Mahakama (MAHAKIMU) kuandika
Barua na kuiwasilisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa..
Akiongea katika viwanja vya Nyerere Square
Jijini Dodoma ambako Maadhamisho ya wiki ya Sheria yanafanyika, Naibu Katibu wa
Tume ya Utumishi wa Mahakama (Nidhamu na Maadili) Bi. Alesia Mbuya amewataka
wananchi kutokuwa na wasiwasi wanapoona hawakutendewa haki na Mahakimu kutokana
na ukiukwaji huo.
Bi. Lesia amesema Wanachi wanapaswa Kuandika Barua za
Malalamiko hayo na kuziwasilisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa au Wakili
anayetoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu Serikali.
Amesema barua hiyo ikishapokelewa na katibu wa kamati
ya Maadili ikawa imekithi vigezo vikiwemo kusainiwa na Mlalamikaji
na kisha hufanyiwa uchunguzi dhidi ya Hakimu mlalamikiwa, baada ya hapo
Jarada hufikishwa mbele ya Wajumbe wa Tume wa maadili kwa ajili ya Kufanyiwa
maamuzi
" Mwananchi asiwe na woga, kama anaona hakutendewa
haki mahakamani na Hakimu kutokana na ukiukwaji wa maadili, aandike barua ya malalamiko
kisha aifikishe Ofisi ya Mkuu wa mkoa kwa Katibu Tawala itafanyiwa kazi
na kamati kisha italetwa tume na kufanyiwa maamuzi", amesema
Aidha amesema inapobainika Hakimu amekiuka Maadili ya
Utumisha wa mahakama kuna hatua anachukiwa ikiwemo, kufukuzwa Kazi,
kusimamishwa au kuonywa hivyo wananchi wasisite.
Naibu katibu Huyo amesema Tume hiyo Imeundwa kwa
ajili ya kuimarisha maadili ya Maafisa mahakama (Mahakimu), ambapo tume hiyo
ina wajibu wa kuziimalisha kamati za maadili kwa kuzijengea uwezo ili ziweze
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
Aidha amesema Changamoto ambayo Tume inakumbana nayo katika utekelezaji wa majukumu Yake, ni pamoja na Wananchi kutofahamu vema majukumu ya Tume hiyo, pamoja na kamati zake, hali inayosababisha wananchi wenye malalamiko dhidi ya ukiukwaji wa Maadili kwa Mahakimu, kutojua Utaratibu na Sehemu Sahihi za kuwasilisha malalamiko Yao dhidi ya ukiukwaji huo.