..........................
Na Rose Jacob,MWANZA.
WATU 8 wamefariki dunia na wengine 39 kujeruhiwa,baada ya Mabasi mawili kugongana wakati yakiwa safarini,katika kijiji cha Ukirigulu wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa ,alisema ajali hiyo iliyohusisha gari aina Asante Rabi iliyokuwa ikitokea Jijini Mwanza na kugonga na gari la Nyehunge,lililokuwa likitokea mkoani Morogoro.
Alisema ajali hiyo imetokea October 22 mwaka huu,majira ya saa 12 asubuhi baada ya gari la Nyehunge kujaribu kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele yake kisha kugongana na gari la Asante Rabi.
Aidha baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema, walishuhudia namna dereva wa gari la Asante rabi alivyokuwa anajaribu kuyapita magari mengine ndipo alipogongana na gari hilo.



