NA JOHN BANDA, ARUSHA
ZAIDI ya Wanawake 200 wa Ushirika wa Mama Wa Kikristo (UMAKI) wa Kanisa Anglikana Tanzania, Wameanza mkutano wao mkuu wa 18, unaofanyika jijini Arusha kunzia leo Sep 5 mpaka 9 2024 unaofanyika katika Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Ukiongozwa na Ujumbe kutoka 3 Yohana 1:2 Usemao "Mpenzi, Naomba Ufanikiwe katika mambo yote na Kuwa na Afya yako, kama vile roho yako ifanikiwanyo",
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo wanawake hao wameanza na Maandano yaliyoanzia katika kanisa la Saint James mpaka Kanisa kuu la Christ Charch Cathdral, jijini humo ambapo yalipokelewa na Askofu wa Dayosisi hiyo Dkt. Stanley Hotay huku kukitarajiwa kutolewa mada mbalimbali zitakazotolewa na Maaskofu na Wamama Askofu waliwemo wataalama mbalimbali.
Katibu wa UMAKI, Margareth Ndonde akifafanua jambo mara baada ya maandamano hayo.
Askofu wa Dayosisi ya Mount Maru Dkt. Stanley Hotay akipokea Msalaba kutoka kwa Mama Askofu Veronica Almas wakati wa mapokezi ya Maandamano.