BANDA MEDIA BLOG

PROF. JANABI ACHAGULIWA MKURUGENZI WHO KANDA YA AFRICA


 Profesa Mohamed Janabi amechaguliwa kuwa Mkurugenzi  wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.

Profesa Janabi amechaguliwa katika mkutano uliofanyika leo Mei 18, 2025 huko Geneva, Uswisi ambapo mataifa wanachama yamepiga kura katika kikao cha pili maalumu cha kamati ya kikanda cha shirika hilo. 

Profesa Janabi anaziba nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri wa zamani wa Afya Tanzania, aliyefariki dunia mwezi Novemba 2024.

Profesa Janabi ni mmoja wa wataalamu wakubwa wa afya nchini Tanzania, akiwa pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG