BANDA MEDIA BLOG

AHMED ALLY ABWAGA ABWAGA MANYANGA


 Umekua msimu mbaya kwetu kwenye michuano ya kimataifa, inauma lakin hatuna budi kukubali kuwa msimu huu umekua mgumu kwetu

Kama ambavyo misimu mingine tunafuzu kwenda Robo Fainali na wengine wanashindwa basi msimu imekua zamu yetu kuanguka

Hatuna sababu ya kuvurugana wala kutafuta mchawi itoshe kusema msimu huu haukuwa wetu au haikua rizki yetu

Tumalizie mechi mbili zilizobaki baada ya hapo tuwekeze nguvu kwenye mashindano ya ndani huku bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri

Poleni ndugu zangu Wana Simba, Tulichozea kufanya tumeshindwa kufanya safari hii,  Tukubali kuwa huu ni msimu mbaya kwetu na hutokea kwa timu yeyote Duniani

Asanteni na poleni wale wote waliotoa nguvu zao kuipambania Simba ishinde hii leo, Asanteni wale wote waliokuja Uwanjani hii leo, Tanatambua na kuthamini mchango wenu kwenye kuipambania Simba yetu

Itoshe kusema Asante Mungu wewe ndio mpangaji wa yote

"hadi wakati mwingine Wanyama, Hakuna kukataa tamaa maisha ya mpira bado yanaendelea", anaandika Semaji la Cuf

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG