Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula (kulia) akizungumza na
wabunge wa CCM kwenye semina maalum ya Wabunge wote wa CCM inayofanyika
kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wengine pichani
ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye (kushoto).
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Ndugu Nape Nnauye (kulia)
akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza Mhe. Shanif
Mansoor muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha wabunge wa CCM kwenye
ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akizungumza
na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni
Mbunge wa viti maalum Mhe. Annastazia Wambura muda mfupi kabla ya kuanza
kwa kikao cha wabunge wa CCM mjini Dodoma.
Tags
SIASA