…………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Good News for All
Ministry, Askofu Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza
kumuomba Mungu dhidi ya hali ya hewa ya joto kali nchini.
Askfou huyo ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar e s Salaam
mara baada ya Mamlaka ya hali ya hewa kuonyesha hali ya joto kufika
nyuzi joto 35°C.
Askofu Gadi ameongeza kuwa,
wanatarajia kufanya mkutano wa maombi siku ya Jumatano ya tarehe 20
Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki maarufu kama Feri ili
kuomba Mungu kuepusha ongezeko la joto nchini.
“Joto limesambaa katika maeneo
ya pwani hususani Dar es Salaam, Tanga, na visiwa vya Zanzibar, hivyo
kwa hali hii tumeona tufanye mkutano wa maombi mafupi katika eneo la
Soko la samaki la feri siku ya Jumatano kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6
mchana,
“Mungu amenipa nafasi ya kuomba
dhidi ya majanga ya kimazingira kama haya hivyo tunawakaribisha watu
wote wa Dar es Salaam tuje tumlilie Mungu kwa pamoja ili tuondokane na
janga hili la joto na madhara ya Elnino” alifafanua Askofu Gadi.
Kwa upande wake katibu wa Good
News For All Ministry Mchungaji Palemo Massawe amewataka Wananchi
kuchukua hatua ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa
kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka.
Uongozi huo unaendelea na
maombi ya kumuombea Rais John Pombe Magufuli kufanikiwa katika juhudi
zake za kulikomboa nchi kiuchumi na kielimu.
Tags
HABARI ZA DINI