Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , wameamia kubadili 'Jenerali' katikati ya vita, Kwa kumchagua Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti mpya wa Chamabhicho.
Lissu ameshinda nafasi hiyo dhidi ya mshindani wake Freeman Mbowe aliuekiongoza chama hicho Kwa miaka 21 katika mkutano wa ucuaguzi ulioanza Jana asubuhi na unaendelea lao Jumatano Januari 22,2025 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es lam.
Uamuzi huo Wa wajumbe, unahitimisha Safari ya miaka 21 ya uenyekiti wa Mbowe aliyepokea wadhifabhuo kutoka Kwa Bob Makani tangu 2003.
Lisu Anakuwa mwenyekiti wa 4 wa Chadema, akitanguliwa na Edwin Mtei, Bob Makami na Mbowe.
Licha ya matokeo ya Jumla kutotangazwa baada ya katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuwaeleza wajumbe wa Mkutano mkuu matokeo yatatangazwa Baadaye, lakini Jumble ni Shangwe limetawala.
Msingi wa Shangwe hilo ni Kura za binafsi ya uenyekiti zimemalizika kuhesabiwa na mawakala wa Lissu kwa namana moja au nyingine wamepenyeza matokeo ya awali.
Katika ukurasa Wa kijamii x wa Mbowe ameandika Ujumbe wa Kukubali kushindwa akiweka na Picha aliyopiga na Lissu na kuandika: " Nimepokea Kwa mikono miwili maamuzi ya ucuaguzi ya ucuaguzi wa mkutano mkui wa chama chetu Chadema ulihitimishwa Leo asubuhi Januari 22,2025. Nampongeza mhe. Tundu Lissu na wenzake Kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Cham. Nawatakia kila la Kheri katika kukipeleka mbele chama chetu".
Ukimya ulitawala Kwa timu inayomuunga mkono Mbowe, huku Ile ya Lissu ikionekana Kufurahia.
Hizo zililuwa Rasharasha za matukio ya ukumbini kabla ya matokeo rasmi kutangazwa, katika ucuaguzi huo
Ulifika wakati wa Wajumbe wanaomuunga mkono Lissu walionekana kukumbatiana, kupeana mikono na kupongezana.
Hatua hiyo ilifuatiwa na furaha inayoashiria ushindi kutoka Kwa baadhi ya wajumbe hao na hawakua wametulia ukumbini.
Wajumbe hao wa Timu Lissu walionekana kukaa vikundi vikundi na mmoja mmoja alichomoka kwenda kwenye kikundi kingine, huku wakinong'onezana na kupeana mikono.
Yote hayo yaliendelea katika kipindi ambacho matokeo Rashmi ya uchaguzi hui hayajatangaza Mbowe, Lissu wala Charles Odero kuwa ndiye Mshindi.
Kwa upande wa wajumbe waliojinasibu kumuunga mkono Mbowe, walikuwa kimya na macho ya wengi yalielekezwa kwenye Runinga zilizokuwepo ukumbini hapo zinaonyesha mawakala wakihesabu Kura.
Dakika chache baadaye, wafuasi wa Lissu walisimama ukumbi mzima na kushangilia, hatua iliyosababisha katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika awaamilishe watulie.
Sambamba na hilo, alitantaza kukamilika Kwa hatua ya kuhesabiwa Kura na wanapaswa kusaini fomu za matikeo wameshafanya hivyo.

.jpeg)