BANDA MEDIA BLOG

HII HAPA IDADI YA KURA ZA TUNDU ANTIPAS LISSU ZILIZOMPA UBOSI CHADEMA

 

Lissu alipata zaidi ya 51% ya kura zilizopigwa kumpa ushindi wa Uenyekiti wa chama Kitaifa / Picha: Tundu Lissu 


JUMLA YA KURA 1014

KURA ZILIZOPIGWA 999
998 KURA HALALI
ZILIZOHARIBIKA 3

ODERO CHARLES amepataKura 1 sawa na Asilimia 0.1℅
FREEMAN MBOWE: amepata Kura 482 sawa na Asilimia 48.3℅
TUNDU LISSU: amepata Kura 513 Asilimia 51.5%

MATOKEO MAKAMU MWENYEKITI BARA

JUMLA YA KURA 1014
KURA ZILIZOPIGWA 1005
KURA HALALI 998

Lissu ametangazwa mshindi mapema leo Jumatano, Januari 22, baada ya shughuli ya upigaji kura uliofanyika usiku kucha katika mkutano wa wajumbe wa taifa wa chama hicho, jijini Dar es Salaam.

''Ushindi huu ni wetu sote!'' aliandika Lissu katika ukurasa wake wa X muda mfupi baada ya matokeo kujulikana.

Katika mkutano huo, John Heche alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa baada ya kukusanya zaidi ya 57% ya kura.

Mwenyekiti anayeondoka Freeman Mbowe alikuwa wa kwanza kukubali matokeo ya kura hizo na kumpongeza mshindani wake.

''Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025,'' amesema Mbowe. ''Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu.

Chadema Party

Freeman Mbowe amekuwa mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA tangu Septemba 14, 2004. Anasifiwa kwa mabadiliko mengi yaliyotokea ndani ya chama kwa miongo miwili iliyopita, na kuahidi kuleta zaidi iwapo ataendelea kukitumikia chama kama mwenyekiti wake wa taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG