BANDA MEDIA BLOG

WANAFUNZI WAFURIKA BANDA LA HESLB KUPATA ELIMU YA MIKOPO

 Zanzibar, Julai 18, 2026

Mamia ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya kati na vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2026/2027, wanaendelea kutembelea kwenye banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ili kupata elimu ya jinsi ya kuomba mikopo kwa usahihi.

HESLB ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwenye Maonesho ya 7 ya Wiki ya Elimu ya Juu Zanzibar yaliyoanza Julai 14, 2026 na yatahitimishwa Julai 20, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja. 

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia amepata fursa ya kutembelea mabanda ya wadau mbalimbali likiwemo la Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar ili kujionea bunifu na huduma nyingine zinazotolewa. 

Katika maonesho hayo ambayo yana kauli mbiu isemayo, *”Ubunifu na Taaluma ni Msingi wa Maendeleo”*, HESLB inatoa elimu ya utoaji mikopo ikiangazia zaidi sifa na vigezo kwa mwaka huu 2026/2027 na pia kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa mikopo iliyoiva. 

Baada ya Unguja, yatafuata Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu Pemba kuanzia Julai 23 hadi Julai 27, 2026 katika Uwanja wa Gombani.   

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG