NA JOHN ISRAEL, DODOMA
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni nchi pekee Duniani iayotoa
cheti cha Ndoa kwa wanandoa Bila wahusika kuwa na Elimu Stahiki hali
inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika mahakamani hasa za wakristo.
amesema 2=1 imekuja kuponya ndoa na kanisa la
Tanzania kwani nchi hiyo ndiyo nchi pekee inayotoa vyeti vya ndoa bila wahusika
kuwa na elimu ya kada hiyo nyeti ambayo ni chanzo cha kila kitu kwenye familia,
Jamii, Taifa na Dunia kwa ujumala
Dkt. Yuda amesema kuwa wakati alipokuwa akichukua shahada
ya Udakitari alibaini kwenye nchi 17 alizofanya utafiti kwenye eneo la uhusiano
kuwa ndoa hasa za wakristo wakiwemo viongozi wa dini hiyo zinaongoza kuvunjwa
mahakamani.
“ni Tanzania pekee inayotoa cheti bila wahusika
kumaliza mafunzo kwenye kada ya ndoa ambako wahusika hufika madhabahuni
wanavalishana pete, kwa maneno machache ya msajili wa ndoa hiyo kisha wanakabidhiwa
vyeti bila hata kujua kwenye ndoa kuna nini
Adha amesema elimu nyingine zote lazima mtu asome afanye
mtihani afaulu ndipo apate cheti husika lakini kwenye Ndoa si hivyo
‘’nilipokuwa nikifanya utafiti wakati nilipokuwa
nikichukua shahada ya yangu ya udaktari, katika nchi 17 za Africa niligundua, Ndoa
zinazoongoza kuvunjwa mahakamani ni za wakristo huku wengi wao wakiwa viongozi
wa dini hiyo wakiwemo maaskofu, wachungaji, wazee wa kanisa na wengine’’, amesema
Akiongea kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa 2=1 Ministries Africa Gavin Moses na Ammelia moses amesema ili amani na usalama viwepo kuanzia ngazi ya familia, jamii, Taifa na Dunia kwa ujumla ndoa zote zinamhitaji Mungu.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa 2=1 Ministries Tanzania Askofu
Amos amesema huduma hiyo imezaliwa upya, kwani awali watu waliaminishwa
kuanzishiwa Miradi bila kupewa maarifa, lakini sasa maarifa kwanza ndipo miradi
ifuate.
Katika kongamono hilo lililoongozwa na Mkurugenzi wa huduma
ya 2=1 Africa Gavin na mke wake Ammelia kutokea nchini Africa Kusini, pia
ulihudhuriwa na maaskofu nane toka nchini Congo DRC, ambapo uongozi wa taifa la
Tanzania umewasisitiza washiriki wote kuwa watapata maelekezo ya hatua zitakazofuta
kutoka kwa viongozi wa mkoa wa Dodoma unaoongozwa na Askofu Dkt. Elia Mauza.