MALIKIA wa nyimbo za injili Nchini Tanzania Rose Muhando anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni huko nchini Kenya na mwimbaji mwenzake wa nyimbo za injili.
kwa mujibu wa mitandao ya kijamii nchini humo Malikia huyo anatarajia kuolewa na Bishop, Robert Bob Lumbasi ambapo Bishop huyo ametoa tangazo rasmi kuwa, Rose Mhando hayuko sokoni tena bali kwa sasa anasubiri kuolewa kwani kila kitu kipo tayari, na kwamba hata mahali tayari zilishatolewa zote
Imebainishwa katika vyanzo hivyo kuwa Wapenzi wa Muziki wa Injili wa wawili hao, wanasubiri kwa hamu Tarehe ya harusi hiyo, ambayo inatajwa kuwa itakuwa ya kukata na shoka kwani watarajiwa hao ni watu maarufu huku Bob akitajwa kuwa ni Afisa wa Polisi, Bishop na mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini humo.
