Mwalimu Doris Peter akiwa kwenye majukumu yake
UALIMU ni wito, pia ni kazi kama zilivyo kazi
nyingine za kitaaluma si kazi za watu waliopotea au kufeli Maisha usione
mwalimu anaongea kwa sauti ya juu, kwa vitendo vya mikono na hata mwili mzima
wakati mwingine akiimba na kucheza Pamoja na wanafunzi wake ukamchukulia poa.
Mnachotakiwa kujua ninyi madaktari, Wahandisi, Tehama,
Waongozaji wa Ndege, Meli na wa huko jeshini, Waandishi wa Habari, Wanasayansi na
wengine ambao sijawataja hapa. Wote tulipita mikononi mwa walimu bila kujali
hali na mapito yao ya kimaisha yalikuaje.
Hapa BANDA MEDIA tumekutana na Mwalimu Doris Peter
anayefundisha Shule ya Msingi Yusufu R. Makamba iliyopo Wilayani Temeke jijini
DSM, aliyepata nafasi ya kutusimulia hadithi yake ya alipotoka mpaka kufikia
Kuwa kiongozi wa Fikra katika Ualimu.
Mwalimu huyo anasema baada ya kumaliza kidato cha nne
katika shule ya sekondari ya Vituka mwaka 2007, alianza kazi ya kuuza Duka la
Baba mmoja aliyekuwa Jirani yao ambapo hata hivyo mnamo Mwaka 2008 alilazimika
kuiacha kazi hiyo akidai kukimbia uzalilishwaji kingono uliokuwa ukimnyemelea kutoka
kwa Bosi wake huyo.
“nililazimika kuacha kazi hiyo kutokana na kukumbana
na uzalilishashwaji wa kingono tena kutoka kwa bosi wangu mwenye umri mkubwa
kama Baba yangu,
baada ya kumkatalia aliamua kuanza kuninyanyasa na
kuninyima mshahara wangu. Niliamua kuondoka badala ya kupoteza heshima yangu.
Nilijisikia kupungukiwa, lakini kwa hakika nilikuwa najinusuru”, anasema kwa
hisia
Aidha DORIS aliamua kujiunga na Dada yake aliyekuwa
fundi wa kushona nyumbani kwao, akajifunza kushona chini yake baada ya kujua naye
akawa anawafundisha wenzake tena kwa upendo mkubwa, kitendo kilichomfanya Dada
yake huyo anayeulikana kwajini la Jane, kung’amua kipaji cha Ualimu ndani yake,
akaamua kumshauri akasome Ualimu.
“sikuwahi kusoma chuo cha ushonaji bali nilijifunza chini ya dada Jane pale nyumbani, na ndiye aliyenishauri kusomea ualimu baada kuona ninavyowaelekeza wanzangu kushona kwa umakini mkubwa na kwa upendo”, amesema
Mnamo mwaka 2009 alijiunga na chuo cha ualimu Mpwapwa
na kuhutimu ngazi ya cheti mwaka 2011, ambapo mwaka uolifuata wa 2012 alipata
ajira ya kwanza katika shule ya msingi Saku mbagala alipofanya kazi mpaka 2017
na baadae kuhamishiwa shule ya msingi kiwanja cha ndege hadi 2025
alipohamishiwa Yusufu R. Makamba huko Temeke, ambako yupo hadi sasa akiwa mwalimu
wa kawada.
Mwalimu Doris anasema mpaka leo anashindwa kusahau pigo
la kumpoteza kaka yake wa Pekee Mwaka 2016, hali iliyosababisha huzuni kubwa na
mzigo wa Maisha na hali ya upweke kuongezeka
kutokana na wao kuzaliwa watu tu kwa
wazazi wao.
Anaongeza kuwa akiwa kazini , aliamua kujiendeleza
kielimu ambapo Mwaka 2021 hadi 2023 alisoma
uongozi katika Chuo cha ADEM, kwa ajili ya kujengea uwezo wa Uongozi wa elimu. Badala
ya kuwa mwalimu wa Darasani tu bali kuwa kiongozi wa Fikra katika Elimu na kujinyakulia cheti cha Diploma
Mwalimu Doris anatanabaisha kuwa, Ndoto yake kubwa ni
kusoma hadi kufikia ngazi ya Daktari (PhD) au Profesa katika masuala ya Elimu.
“natamani kusoma kwa kengo la kuja kuchangia kwenye
sera, mitaala na mifumo ya elimu inayotambua kwamba wanafunzi hawaji darasani
wakiwa tupu wanakuja na historia, maumivu, malezi, umasikini, upweke na ndoto”,
anasema na kuongeza
anasema changamoto za kiuchumi zinamsababisha kuiona
safari hiyo ionekane ngumu, lakini anaamini ndoto inayozaliwa kwenye maumivu
huwa na nguvu ya kipekee, hivyo ataendelea kusonga nayo mpaka atoboe.
Mwalimu huyo ambaye Pamoja na Ualimu, pia ni mama wa Watoto watatu, anayejua uchungu wa kulea, peke yake ( Single Mother), anajua maumivu kejeli za walimwengu, shinikizo la kimapenzi, mzigo wa kiuchumi, na uchovu wa kuwa mama na baba kwa wakati mmoja. Lakini pia anajua nguvu ya mwanamke asiyekataa haanguki.
Anasema kitu cha ziada kwake ni kuwa mwalimu anayewaelewa
Watoto kwa kina hasa wanaopitia maumivu ya kimya kimya kwa kuwaangalia na hivyo kuchukua hatua ya kuwasaidia kisaikolojia.
Anaweka wazi ndoto yake kuwa bado anaota kuona Elimu
inayojenga fikra, maadili na nidhamu. atamani kuwa mwalimu atakayegusa jamii,
na kuanzisha au kufanya kazi na taasisi itakayosaidia Single Mothers na watoto
wanaolelewa na mzazi mmoja, ili kizazi kijacho kipate msaada na mwanga zaidi.
Hata hivyo Pamoja na yote hayo anapenda kujiendeleza
kwa kusoma makala, vitabu ikiwemo kufuatilia majarida mbalimbali Pamoja na kuandika makala mbalimbali ambazo
zinaweza kuleta matokeo chanya katika jamii na kuwavusha wengine mahala
wanapopita ama kuwasaidia kwa namna moja au nyingine, ikiwemo kuwafariji.
Kwa waliokata tamaa mwalimu Doris anatumia misemo hii
kusema, Kuanguka si mwisho bali ni daraja.
Kama yeye aliyelelewa bila baba, akapoteza kaka, akapitia unyanyasaji wa kingono, akakosa matokeo, akalea watoto peke yake bila mwenza na bado akasimama, wewe pia unaweza kusimama tena amua kuamka leo
uanze moja na mia inakuta
Hata ukianza gizani, unaweza kuwa taa kwa wengine.
Hata ukiumia, unaweza kuwa uponyaji wa wengine.
Na hata ukiwa peke yako, bado unaweza kujenga kizazi.
Safari bado inaendelea kubwa ni kuondoa uoga na
kuianza.
MWISHO





