Rais Mh. Dk. John Pombe Magufuli
akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaa leo kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika
hivi karibuni, Rais Dk. John Pombe Magufuli ameapa katika sherehe
iliyohudhuriwa na marais mbalimbali wa Afrika wakiwemo Robert Mugabe wa
Zamibabwe, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Joseph Kabila wa DRC Congo, Paul
Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyata wa Kenya,
Philipe Nyusi wa Msumbiji, Edgar Lungu wa Zambia na wengine wengi
wakiwemo mabalozi wa mataifa ya Ulaya, Marekani na taasisi za kimataifa
ambao wameshuhudia sherehe hizo.
Dk.John Pombe Magufuli anakuwa
rais wa awamu ya tano baada ya kupokea kijiti kwa watangulizi wake
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee
Benjamin Mkapa na sasa Dk. Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyemuachia
kijiti Dk. Magufuli.
Dk Jakaya Kikwete akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za kumuapisha Rais Dk. John Pombe Magufuli.Rais Dk. John Pombe Magufuli akipokea vitendea kazi kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande mara baada ya kuapishwa kwenye uwanja wa Uhuru leo, anayeshuhudia kushoto ni Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete
Rais Dk. John Pombe Magufuli akipokea silaha za kijadi kutoka kwa mmoja wa wazee Mzee Job Lusinde mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akionyesha silaha za kijadi alizokabidhiwa mara baada ya kuapishwa kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa wamekaa mara baada ya kula kiapo kuitumikia nchi kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mstaafu Dk. Gharib Bilal na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa Rais kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Tags
HABARI KITAIFA

























