Na. Lilian Lundo – Maelezo
Jeshi la Polisi kanda maalum ya
Dar es salaam imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 7 wakiwa na silaha 8
na risasi 62 kwenye msako uliofanyika jijini Dar es salaam katika
kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Jeshi la Polisi kanda maalum ya
Dar es salaam imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 7 wakiwa na silaha 8
na risasi 62 kwenye msako uliofanyika jijini Dar es salaam katika
kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akiongea na waandishi wa habari
leo , katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa
Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amesema wahalifu
walidhani kuwa Jeshi la Polisi limeweka nguvu katika uchaguzi mkuu na
kusahau kufanya misako yake iliyokuwa ikifanya mara kwa mara kama moja
ya majukumu yake.
“Ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi
lilijipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na
misako mingine inaendelea kufanyika kama kawaida kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama na mikoa ya jirani” Alisema kamanda
Kova.
Kamanda Kova aliongezea kwa
kusema kuwa, Jeshi la Polisi kanda maalum inashirikiana na mikoa ya
jirani kuhakikisha kuwa watuhumiwa hao hawapati fursa ya kukwepa mkondo
wa sheria.
Aidha alizitaja silaha
zilizokamatwa kuwa ni SMG moja (1), Bastola sita (6) na Mark 4 riffle
moja (1) na risasi 62 ambapo mpaka sasa jumla ya majambazi 74
wamekamatwa ikiwa ni pamoja na silaha 51 na risasi 890 za silaha
mbalimbali
Kamanda Kova amezidi kufafanua
kuwa kutakuwa na msako mwingine mkali kuelekea sikukuu za x-mass na
mwaka mpya 2016, utakayofanyika katika mikoa ya kipolisi ya Ilala,
Kinondoni na Temeke wakisaidiwa na vikosi maalum vilivyopo Kanda ya Dar
es Salaam.
Msako huo utajikita katika
kuwakamata majambazi, magaidi, wanaojihusisha na madawa ya kulevya,
vibaka, wapiga debe, wanaouza pombe haramu, madanguru yote ambayo pia
huhifadhi wahalifu.
Tags
HABARI KITAIFA