TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO
VYA HABARI TAREHE 03.11.2015.
Kuna
taarifa na ushawishi unaoendelea wa baadhi ya wanachama, Wafuasi wa Vyama vya
Upinzani kutaka kufanya maandamano waliyoyaita yasiyo na kikomo.
![]() |
| RPC MISIME |
Najua wananchi wa Dodoma wangependa
kufahamu nini tamko au wito wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuhusu ushawishi
huo ambao ni kinyume cha sheria na wenye lengo la kutaka kuvuruga amani.
Kwanza
niseme hakuna maandamano yatakayoruhusiwa katika Mkoa wa Dodoma, yenye lengo la
kupinga uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015.
Pili
hayataruhusiwa kwa sababu kulingana na matamshi, maandalizi na uhamasishaji
wake una viashiria vilivyo dhahiri kuwa lengo lake ni kuleta vurugu
itakayopelekea kuvuruga amani.
Tatu
kulingana na sheria, kanuni na taratibu
za Uchaguzi kama kuna mwenye malalamiko yaliyodhahiri na ya msingi zipo njia za
kufuata na siyo kufanya maandamano yasiyo na kikomo.
Nitoe wito kwa Wananchama, Wafuasi wa vyama
hivyo na wananchi kwa ujumla kutojihusisha katika maandamano hayo kwani
atakayefanya hivyo atakabiliwa na mkono wa dola kwa nguvu zote kwa mujibu wa
Sheria za nchi na asitokee wa kulaumu kwani atakuwa amejitakia mwenyewe.
Mwisho
Wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo kama kawaida kwani Jeshi la Polisi Dodoma limejiandaa ipasavyo
kuwalinda wanao tii sheria bila shuruti na kukabiliana na watakao kaidi kutii
sheria bila shuruti.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi - Misime D.A (SACP)
Tags
HABARI KITAIFA

