Kwa
takribani Wiki mbili sasa, Mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali kupanda
katika Soko Kuu la Jijini Mwanza umeendelea kuwaliza watumiaji
wa soko hilo.
Mmoja wa wauzaji wa nyama katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo
Mmoja wa wauzaji wa nyama katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo
Bei ya Nyama imepanda bei maradufu
Mteja akiteta na mwanahabari juu ya mfumuko wa bei katika Soko Kuu la Jijini Mwanza
Shughuli za kibiashara katika Soko Kuu Jijini Mwanza zikiendelea
Mmoja wa akina mama wanaouza chakula Soko Kuu Jijini Mwanza anasema kuwa mfumuko huo wa bei umesababisha biashara zao kukamwa
Kushoto ni Mwenyekiti wa Soko Kuu Jijini Mwanza Hamad Ntola akizungumza na Mwanahabari ofisini kwake juu ya mfumuko wa bei katika Soko hilo
Na:George Binagi-GB
Pazzo
Mfumuko
huo unalalamikiwa na pande zote mbili kwa maana ya wauzaji na wanunuaji
sokoni hapo, ambapo wameomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kiweka
mambo sawa.
Bei kwa
nafaka zote sokoni hapo zimepanda bei hadi shilingi 1,000 kwa kila moja
tofauti na hapo awali ambapo bidhaa iliyokuwa ikiuzwa shilingi 15,000
sasa inauzwa kati ya 2,000 hadi 2,500 ambapo steki ya nyama imepanda bei
kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 8,000 huku nyama mchanganyiko
ikiuzwa shilingi 6,000 kutoka 4,000 za awali.
Mwenyekiti wa Soko hilo Hamad Nchola amesema kuwa mfumuko huo
umesababisha na mazao ya wakulima kupungua katika maghala yao kutokana
na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa mavuno kutokana na ukosefu wa mvua
katika msimu uliopita, pamoja na wafanyabiashara kutoingiza sokoni
bidhaa katika kipindi cha uchaguzi mkuu, ambapo amewasihi
wafanyabiashara kurejea katika mzunguko wao wa biashara kama kawaida
hatua ambao itasaidia kukabiliana na mfumko huo wa
bei.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza
hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapoMmoja wa wauzaji wa nyama katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo

Tags
BIASHARA