BANDA MEDIA BLOG

VAZI LA KHANGA LAFANA KATIKA TAMASHA LA KITCHEN PARTY GALA.

 Wanawake wakiwa wamevalia khanga ambayo ndio ilikuwa dress code ya tamasha walikusanyika kwa wingi kwa ajili ya kupata mafunzo na ushauri bila kusahau burudani. 

Jumapili iliyoisha ya tarehe 08.11. 2015, wanawake mbali mbali jijini Dar es salaam walikutana katika tamasha la kitchen party gala likiwa limebeba ujumbe wa mwanamke simama na timiza ndoto zako. 
Ilichezeshwa droo ya kushinda safari ya Afrika Kusini kwa siku mbili alishinda, iliyodhaminiwa na kinyago tours. Pamoja na droo ya kumtafuta Mshindi wa safari ya Mikumi national park nae alipatikana akapokea certificate toka kwa mkurugenzi wakinyago tours bi Diana
 Pichani juu ni washiriki wa kitchen party gala wakifuatilia mafunzo kwa umakini.
Msemaji Bi Mariam Mbewa Mkurugenzi wa green investment akielezea safari yake ya mafanikio na kuwafundisha kinamama umuhimu wa kuweka akiba.kitchen party gala wakifuatilia mafunzo kwa umakini huku wakiwa na furaha tele juu ya kile kinachoelezewa kutoka kwa Msemaji.
Mwalimu wa masuala ya biashara na ujasiriamali Bryson Makena nae alitema cheche zake na kuwafundisha kina mama kujitambua na ujue kusudio lao hapa duniani ni lipi.
Mkurugenzi wa kinyago tours bi Diana nae alitoa funzo la kufanya kazi kwa malengo hata kama umeajiriwa malengo yako ni yapi?leo ukiachishwa kazi ghafla umejipangaje? ana miaka 27 tu lakini anamiliki kampuni yake ya Tours and safars.

Msemaji Bi Maida Waziri mkurugenzi wa Ibra Contractors nae alishirikisha wanawake safari yake ya mafanikio toka akiwa fundi cherehani mpaka sasa anamiliki kampuni kubwa ya ujenzi wa majengo na bara bara.Aliwasisitiza wanawake kujiamini na kutokuogopa kuthubutu ukijiamini popote unapenya lakini lazima uwe na malengo na mikakati.
Waandaaji wa women in balance kitchen party gala Mtangazaji wa E fm Dina Marios na Vida Mndolwa wakigonga chears kufungua shughuli.
Muongoza shughuli Dina Marios akisisitiza jambo
Ilichezeshwa droo ya kushinda safari ya Afrika Kusini kwa siku mbili na huyu dada ndio alishinda.Atasafiri na mumewe mtarajiwa na imedhaminiwa na kinyago tours.

Mshindi wa safari ya Mikumi national park nae alipatikana bi Edna Haki Ngowi akipokea certificate toka kwa mkurugenzi wa kinyago tours bi Diana

Mchungaji debora akifundisha kina mama kuwa wao ni wasababishaji wanaweza kufanya mambo yasiyowezekana yakawezekana.

Dina marios akipiga selfie na mashabiki wake
PICHA NA DINA MARIOS

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG