Dkt.
Bitrina Diyamett kutoea Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi,
Teknolojia na Ubunifu (STIPRO), akidadavua ripoti ya mwaka 2015
inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa
Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kabla ya
kuzinduliwa rasmi kwa ripoti hiyo.
Akizungumzia
uzinduzi huo, mdadavuzi wa ripoti hiyo, Dkt. Bitrina Diyamett kutokea
Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STIPRO)
alisema katika taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonyesha
jinsi ambavyo Tanzania na nchi nyingine za kiafrika zisivyokuwa na sera
nzuri za viwanda na ubunifu.
Alisema
katika tafiti ambayo imeanza kufanyika mwaka 2000 katika nchi zaidi ya
10 za Afrika kunaonekana serikali za Afrika zinashindwa kutofautisha
sera viwanda na sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu na hivyo
kushindwa kukuza viwanda na kuwasaidia wazalishaji wa nchini sababu sera
hizo ndiyo zinazowaunganisha.
Katika
utafiti huo uliofanywa na UNCTAD unaonyesha kuwa mauzo ya bidhaa
zinazotengenezwa kwa teknolojia ya juu umefikia asilimia 52 mpaka 2014
na umekua kwa asilimia 18 duniani kote kuanzia mwaka 2000 na Afrika
umekua kwa asilimia 0.3 kati ya asilimia 18 ambazo zinaonekana kukua
tangu 2000.
Aliongeza
kuwa ili sera hizo zifanye kazi zinahitaji kushirikiana lakini kwa
Afrika hakuna ushirikiano na kuwa katika wakati mgumu ya kuzifanyia kazi
sera hizo.
 |
| Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, Dkt. Bitrina Diyamett na Bw. Bernard Achiula kwa pamoja wakionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na wanahabari. |
“Wamefanya
utafiti lakini Afrika hali sio nzuri shida zilizopo hakuna ushirikiano
kila mtu anakuwa kivyake, hawa wanafanya kazi kwa kuangalia sera yao
kivyao na hawa wanafanya kivyao kwahiyo kufanikiwa inakuwa shida,
”
Ukiangalia kwa Afrika hata katika nchi ambazo zinajitahidi kwa sera hizo
kuwa sehemu moja lakini watekelezaji wake hawana umoja kwamba wakae
pamoja kuona jinsi wanafanya sasa unakuwa kama ugomvi kila mtu kuona ni
sera yake na hakuna kitu kinafanyika,” alisema Dkt. Bitrina.
Dkt.
Bitrina alisema kutokuwepo kwa ushirikiano kunafanya kupotea kwa fedha
nyingi kwa sababu serikali inakuwa inatoa pesa nyingi kutekeleza sera
moja na ikitoa tena pesa nyingine kwa utekelezaji wa sera nyingine
lakini kama sera hizo zikifanya kazi kwa kushirikiana kuna uwezekano wa
kuokoa pesa hizo.
Aidha
alitoa ushauri kwa serikali kupitia upya sera ya viwanda na sera ya
sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuzifanya sera hizo kufanya kazi kwa
pamoja na kuweza kuinua viwanda ambavyo ndiyo vinatoa ajira nyingi na
kama watafanya hivyo wataweza kupambana na ukosefu wa ajira nchini na
kuokoa pesa nyingi.
|