Dkt Dorothy Gwajima waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum akiandika kwenye ukurasa wake ameonyesha kushangazwa na umri wa kuishi wa Banadamu walioishi karne za nyuma wa maiaka 900 huku karne zetu umri Ukishuka mpaka maika kati ya 70 na 80 ambapo kutokana na maendeleo ya Binadamu watu wanajichanganya...
"Kuna wakati nawaza kuwa, kadri mwanadamu anavyoendelea kuishi na kupata maendeleo, ndiyo kadri anavyomsahau Mungu na kujivisha ukichaa fulani na matokeo yake Mungu naye ndiyo kadri anavyopunguza miaka yake ya kuishi kwa kuiondoa neema ya ulinzi wake dhidi ya majanga mbalimbali,
Hivi inakuwaje binadamu wenzetu karne zilipita waliishi kwa heshima na adabu wakafikisha Mungu akawatunikia hadi miaka 900 karne zetu sisi ikabakia 70 na tukiwa ambapo tukiwa na nguvu ni maiaka 80? na bado pamoja na muda huu mdogo tunapata na muda wa kuvurugana na kuvuruga maadili na kushusha heshima ya utu wetu tuliopewa na Mungu kwamba tunafanana naye na kusababisha majanga na vifo achilia mbali kuvuruga mazingira hadi tabia nchi inabadilika.. ???
Hivi, si Mungu atapunguza tena miaka ? Halafu sasa lini utazaliwa, ukue, usome, uzae, utunze watoto wako?
Shauri yako, mimi simo kati ya wavurugao maadili", amesema na kushari, Dkt Dorothy Gwajima Waziri anayehudumu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Sema mimi simo👋Hatumo.

