BANDA MEDIA BLOG

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LASHUTUMU SHAMBULIO KATIKA UBALOZI WA SAUDI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeshutumu shambulio katika ubalozi wa Saudi Arabia Jijini Tehran lililofanywa na waandamanaji wenye hasiri kufuatia kuuwawa wa kiongozi wa dhehebu la Shia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya baraza hilo haikugusia mahala popote kitendo cha kutekelezewa adhabu ya kifo cha Sheikh Nimr al-Nimr na serikali ya Saudi Arabia.

Siku ya jumatatu, Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki, Numan Kurtulmus ameyasihi mataifa ya Iran na Sauri Arabia, kutuliza mgogoro huo unaoitikisa eneo la Mashariki ya Kati.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG