Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii Tanzania (RCSDS),Abraham Shempemba ( kulia ) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya tafiti zao walizozifanya zinazoonesha takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji wa jamii na jinsi ilivyonufaika. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kituo hicho, Chrizostom Thadeo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
KITUO cha Utafiti wa shughuli za maendeleo ya jamii Tanzania(RCSDS), kinatarajia kuzindua mfumo wa kielektroniki wa kukusanya, kuhifadhi na kuweka angani taarifa za kitafiti za uwajibikaji wa taasisi za binafsi, za umma na watu binafsi serikali kuu na za mitaa na hata mtu mmoja mmoja.
Mfumo huo
unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo utapelekwa katika
mikoa 30 Tanzania Bara pamoja na maeneo 100 yenye wananchi wenye
uhitaji mkubwa.
Akizungunza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Abraham Shempemba alisema lengo la mwendelezo huo ni kutoa nafasi kwa walengwa kutambua mchango unaotolewa kwao na wadau mbalimbali pamoja na misaada kwa jamii zenye uhitaji mkubwa.
Akizungunza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Abraham Shempemba alisema lengo la mwendelezo huo ni kutoa nafasi kwa walengwa kutambua mchango unaotolewa kwao na wadau mbalimbali pamoja na misaada kwa jamii zenye uhitaji mkubwa.
"Sisi
kama RCSDS tunatambua uwepo wa makampuni, mashirika na taasisi
mbalimbali za umma na binafsi zinazochangia kwa kiasi kikubwa mahitaji
na hata majanga yanapotokea ili kunusuru na kuboresha maisha ya
watanzania wenzetu na kuthamini michango na misaada yao,"alisema.
Alisema
mfumo huo unaoaznishwa una lengo la kutambua michango na misaada
mbalimbali inayotolewa na wadau kwa jamii pia wadau nao wapate fursa ya
kuweka malengo yao ya uwajibikaji kwa jamii kwa kuona ni wapi wanaweza
kuwekeza zaidi kiuwajibikaji na eneo lipo nani amewekeza.
Shempemba
alisema utafiti walioufanya na kuutolea taarifa msimu ulipita kwa
kushitikiana na taasisi ya ukaguzi ya Konsalt inayofanyika kila mwaka
wapo waliosaidia jamii kwa sekta mbalimbali kama huduma za afya, maji,
miundombinu, elimu, michezo, maafa na mambo mengine kwa asilimia
tofauti.
Aliongeza
kuwa tafiti hizo pia zimesaidia takwimu za misaada iliyotolewa kisekta,
gharama zilizotumika, uwajibikaji jamii ulivyowekezwa, jamii
ilivyonufaika na misaada hiyo na wadau walivyonufaika na uwekezaji wao
kwa jamii hizo.
Tags
UTALII