Serikali imesimamisha shughuli za
uchimbaji wa Makaa ya Mawe ya Kampuni ya Off- Route Technology iliyopo
Kyela ikiwemo kukamata vifaa vya uchimbaji na kuwekwa chini ya uangalizi
wa Mkoa wa Mbeya hadi hapo uchunguzi dhidi ya uhalali wa kampuni hiyo
kuchimba makaa utakapokamilika.
Hatua hiyo inafuatia ziara ya
Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutembelea mgodini
hapo na kubaini kuwa, kampuni hiyo inachimba makaa bila kuwa na leseni
halali ya uchimbaji madini.
Aidha, Prof. Muhongo ameitaka
kampuni hiyo kulipa kodi zote za Serikali ikiwemo inazodaiwa na
Halmashuri tangu ianze kufanya shughuli za kuchimba. Aidha, ili kujua
undani wa suala hilo, Prof. Muhongo ameitisha kikao kifanyike kati ya
mgodi huo , Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania ( TMAA), Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi, Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kyela, tarehe 18 Januari, 2016
Tags
HABARI KITAIFA