Naibu Waziri wa
Afya Ustawi wa Jamii Jinsia Watoto na Wazee Dk Khamis Kigwangala
akizungumza na Abdul Juma Ofisa Huduma wa Mpango wa wa taifa wa Damu
Salama (NBTS)wakati alipotembelea katika taasisi hiyo Ilala jijini Dar
es salaam na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika taaisis
hiyo pamoja na changamoto zinazoikabili taaisis hiyo, Katikati ni Dk.
Adelin Mgasa Meneja wa Kanda ya Mashariki.
Naibu Waziri wa
Afya Ustawi wa Jamii Jinsia Watoto na Wazee Dk Khamis Kigwangala
akimsikiliza Abdul Juma Ofisa Huduma wa Mpango wa wa taifa wa Damu
Salama (NBTS) wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu shughuli
zinazofanyika katika taaisis hiyo, kulia ni Dk. Adelin Mgasa Meneja wa
Kanda ya Mashariki.
Baadhi ya
wataalam wakipima damu iliyokwisha kusanywa kutoka vituo mbalimbali
jijini Dar es salaam ili iweze kuchujwa na kuhifadhiwa na tayari kwa
matumizi ya wagonjwa katika hospitali mbalimbali jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo –MAELEZO.
Serikali
imezitaka kila halimashauri nchini kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya
kutosha kwa ajili ya damu ili kuwezesha wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo
kuipata na kuepusha kupoteza maisha ya watu hususan wakina
mamawajazwazito na watu waliathirika na ajali.
Aidha Serikali
imesema damu hutolewa bure, hivyo mtu yoyote atakayeuziwa damu ataoe
taarifa kwa mkuu wa wialaya , mkuu wa mkoa au wizarani ili wahusika
waeze kuchukuliwa hatua. Hivyo Watanzania wasikubali kutoa rushwa kwa
ajili ya kupata damu.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala aliyoifanya leo katika Ofisi za
Mpango wa Taifa wa Damu zilizopo jijini Dares Salaam.
Awali
akitembelea ofisi hizo, Dkt Kingwangala alielezwa na Dkt . Avelina
Mgasa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni
halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo.
“ Mganga Mkuu au
Mkurugenzi ambaye ahatawajika kukaikisha damu inakuwepo katika vituo
vya kutolea huduma ataripotiwa kwa mmlaka zilizomteua ili ziweze
kumchukulia hatua,” alisema Dkt. Kingwangala.
Dkt. Kingwangala
aliitaka mifumo ya bima nchini kuhakikisha iligharamia mifuko ya
kuhifadhi damu na reagent(vitenganishi) kwa wagonjwa waowalipia huduma
za afya ili kuweza kusiadi changamoto inayoikabili ofisi hiyo.
Aidha Dkt.
Kingwangala aliitaka ofisi hiyo kuwa na mfumo wa kieletroniki wa
kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao
zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa
wachangiaji endelevu.
Tags
AFYA