Meneja
wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo
(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 afisa uhusiano
wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Amani
Center ,Kampuni ya Tigo imetoa kiasi hicho cha fedha pamoja na vifaa vya
michezo kwa ajili ya maandalizi ya mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Meneja
wa kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo akikabidhi fulana
kwa watoto waishio katika mazingira magumu ya Kituo cha Aman Center cha
mjini Moshi.
Meneja
wa Tigo Kanda ya Kaskazini ,Henry Kinabo akifurahia jambo na afisa
uhusiano wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha
Amani Center ,Salma Khatibu,wengine ni watoto waishio katika kituo
hicho.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Tigo Tanzania leo imetoa mchango wa vifaa vya michezo na pesa taslimu 5m/- kwa kituo kinacholelea watoto wa mitaani cha Amani kilichopo mjini Moshi kukisaidia kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ya mbio za Kili Marathon.
Akiongea
katika makabidhiano ya msaada huo kituoni hapo, Mkurugenzi wa Tigo wa
Kanda ya Kaskazini George Lugata amesema, “msaada huu ni sehemu ya
jitihada mbalimbali za kampuni ya Tigo katika
kuisaidia jamii kukabiliana na changamoto za kimaisha na kuinua hali ya maishaya watanzania kama ilivyoainishwa katika sera yetu ya kuisadia jamii.”
kuisaidia jamii kukabiliana na changamoto za kimaisha na kuinua hali ya maishaya watanzania kama ilivyoainishwa katika sera yetu ya kuisadia jamii.”
Aidha
aliendelea kusema: “Tunaamini msaada huu utaleta tabasamu katika nyuso
za watoto na walimu wa Amani Centre na kuwasaidia kufanya vizuri katika
mshindano ya Kili Marathon.”
Mashindano
ya Kili Marathon ambayo mwaka huu yanadhaminiwa na Tigo pamoja na
kampuni zinginezo, yanafanyika mjini Moshi jumapili ijayo.
Akipokea
msaada huo kutoka Tigo, Mkurugenzi wa Kituo cha Amani Centre,Meindert
Schaap ameishukuru Tigo kwa moyo wa upendo na kuahidi ushindi kwa
washiriki kutoka Amani Centre katika mashindano ya Kili Marathon.
“Tunatoa
shukrani zetu za dhati kwa Tigo kwa msaada huu na tunaamini hii ni
motisha tosha kwa washiriki wetu katika mbio za Kili Marathon kufanya
vizuri na kukipa ushindi na sifa kituo chetu,”alisema Schaap.
Kituo cha Amani centre kilianziswa mwaka 2008 kwa lengo la kuwapa hifadhi na elimu watoto waishio katika mazingira magumu. Mpaka sasa kituo kina jumla ya watoto 71 wakiwemo wavulana 58 na wasichana 13.
Tags
MICHEZO KITAIFA







